Mpya
Loading...

Wafadhili wasitisha kuisaidia Tacaids

Nchi kadhaa za Ulaya na Asia (Japan, Sweden, Ireland, Norway, Switzerland, Uingereza, Ufaransa, Ubelgiji na Uholanzi.)zilizokuwa zikiisaidia Tanzania fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya Ukimwi, zimesitisha msaada wake katika kile kilichoelezwa kuwa, kuiwezesha Serikali kuanza kujitegemea.

Uamuzi huo umekuja wakati  ambapo Serikali imekuwa ikitegemea sehemu ya fedha za wafadhili kutoka Mfuko wa Dunia wa Kupambana na Ukimwi na Kifua Kikuu (Global Fund) kwa ajili ya kuhudumia waathirika na ununuzi wa dawa. 

Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania (Tacaids), Dk Fatma Mrisho alitangaza uamuzi wa nchi hizo kusitisha misaada hiyo na kuitaka Serikali iharakishe mpango wa nchi kuanza kujitegemea.

Dk Mrisho alitoa kauli hiyo  wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala iliyotembelea ofisi hizo zilizopo jijini
Dar es Salaam jana.

Alisema mbali ya nchi hizo, Jumuiya ya Ulaya (EU) na Benki ya Dunia (WB) pia zimesitisha misaada ya Ukimwi kwa
Tanzania.

Dk Mrisho alisema waliobaki ambao wanaendelea kuisaidia
Tanzania kudhibiti Ukimwi ni Marekani na Global Fund.

Alisema ili kukabiliana na hali hiyo, Tacaids iko kwenye mchakato wa kuanzisha Mfuko wa Ukimwi Tanzania.

“Serikali ya Marekani na Global Fund ambao ndio wafadhili wakubwa, programu zao zinaishia mwaka 2013, hatuna uhakika kama wataendelea kutusaidia,” alisema Dk Mrisho.

Aliongeza kuwa shughuli za Ukimwi hapa nchini zinahitaji Sh1 trilioni kwa mwaka, ambapo asilimia 97 ya fedha hizo, zimekuwa zikitolewa na wafadhili.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment