Mpya
Loading...

Living Water Centre - Makuti Kawa idara ya vijana, wachangia damu!

Vijana wa kanisa la Living Water Centre - Makuti Kawe walijitokeza kwa wingi kanisani hapo kuchangia damu katika bank ya damu Hospitali ya taifa ya Muhimbili kwa hiari yao wenyewe. Ni baada ya kugundua kuwa wanaweza kufanyika msaada na kuokoa maisha ya watu wengi wanaopoteza maisha hospitalini kwa kukosa damu. Madaktari na wahudumu kutoka bank ya Damu Tanzania walialikwa katika kanisa hilo baada ya kuombwa na vijana wa hapo baada ya kuamua kuwa wako tayari kuchangia damu.! Damu ni Uhai!
Ilikuwa ni baada ya ibada ya Jumapili ya tarehe 16 Septemba 2011ndo vijana walipoamua kuchangia damu. Na hili litakuwa ni zoezi endelevu.

Mamaaa Happy Donald na yeye kama kawaida mstari wa mbele kabisa na hapa ndo anatoa damu sasa
.
Kabla ya kutoa damu nilazima kwanza kupimwa kama unaweza kutoa au lah! haka kasindano kanaumaa!
Hapa dada Woinde akipata vipimo kabla ya kutoa damu. na pia anapatiwa ushauri,huku mtenda kazi Yusuph akisubiria zamu yake.
Dada Franisca akiwa ame relax kabisa huku akitoa damu

Dada Woinde Muro akiangalia kwa makini damu ikitoka mwilini mwake na kuingia kwenye kifaa maalumu cha kuhifadhia, Ni kama ana imagine jinsi anavyookoa maisha ya mtu mwingine aliyekosa damu. mmmmh Mungu akubariki.
It is so much blessing to be a solution to someone else, to be a hope to the hopeless! Mungu ni mwema, Emcee Hudson Kamoga akitoa damu hapa
Hapa na penyewe kazi haikuwa nyepesi,Davies ndo anatoa damu sasa baada ya hapa jamaa akajipoza na soda kidogo duuuu!
Ilikuwa ni zamu ya Mr Lyamba sasa na hapa ndo mshikemshike ukawadia duuuuuuuuh.........!

M/kiti wa vijana na yeye hakuwa nyuma katika zoezi zima la utoaji damu. Ingawaje anaonekana anaogopa vileee haahahaha!

Wito kwa vijana wengine wote, tuchangie damu,tuokoe maisha ya wengi wanaopoteza maisha kwa sababu tu ya kukosa damu.
Mungu Ibariki Tanzania,Mungu tubariki vijana wa Tanzania. Amen.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment