Mpya
Loading...

Mawazo(Mtazamo) chanya huzaa maisha chanya!


Ninaamini kwamba kila binadamu ameumbwa na uwezo wa kuwa bora au tuseme nyata(star) ing'aayo katika maisha, kila mmoja amezaliwa na uwezo wa kuwa na maisha mazuri.Kila mmoja amezaliwa kuwa mtu mzuri. Maisha mazuri au mabaya ni uchaguzi wa kila mtu,na vyote vinaanzia kwenye mitazamo na mawazo yetu. umaskini au utajiri unaanzia kwenye mfumo mzima wa mtu kuwazo na mtazamo wake kwa ujumla. hakuna mtu aliyezaliwa maskini au tajiri wote tunazaliwa katika hali moja hatuna nguo(uchi) katika usawa.

Japokuwa kila binadamu si mkamilifu kwa sababu tu ni binadamu.



Maisha yanaanza hapo na mitazamo tunayopandikiziwa tunapolelewa inatupelekea kuwa jinsi tulivyo leo,na unao uwezo wa kubadilisha mtazamo na kmazingira yako yatabadilika. Unaweza tu kubadili mazingira yako kwa mtazammo wako,either ukayanya mabaya au ukayafanya mazuri. Kwa hiyo,utaona hakuna wa kumlaumu kama maisha yangu ni mabaya. Ninawajibika moja kwa moja na maisha yangu. Ni kawaida mbaya ya binadamu kutafuta mtu wa kumlaumu maisha yanapokwenda vibaya,wengi hulaumu serikali,viongozi wa dini,wazazi au hata marafiki. Kushindwa kwako au kufaulu kwako ni jukumu lako mwenyewe na hakuna wa kumlaumu.

Mtu ambaye amekulia katika mazingira ya kutosifiwa pindi afanyapo jambo zuri,akili yake imezoeshwa kuonyeshwa vitu vibaya tu alivyo fanya. Mfano,wazazi wake hawajawahi kumsifia labda amependeza,au amefanya vizuri darasani,au katika mazira yeyote tu,mtu huyu anakuwa na mentality ya kutoona vitu vizuri,Akili yake inajengeka katika kuona makosa zaidi kuliko kuona mambo mazuri,anaona zaidi kushindwa na si kushindwa. Hawezi kusifia hata siku moja. Akiona hana la kukosoa,anaona ni bora anyamaze kuliko kusifia. Ukimuuliza,hapa unaonaje,hata sema neno.sababau ya mtazamo wako hasi,na unataka kurushia lawama za kutokujiamini kwako kwa serikali au wazazi. Kulaumu hakutabadilisha uyhalisia kwamba wewe hujiamini,hata kulaumu pi ni ishara ya mtazamo hasi. Unachotakiwa kufanya ni kubadili tu mtazamo na kujitahidi kuona mambo kwa mtazamo chanya. Nina msemo niupendao sana na umenifanya nianze kubadilika sana," We dont see things as they are,we see them as we are" Imenisaidia

Mtazamo wake katika mambo ni hai tu mara zote,kila kitu kwake huwa kinamakosa. Hutoa makosa zaidi kuliko suluhisho.




Mtazamo chanya unamjengea mtu matumaini na kujiamini katika mamabo ayafanyayo. Kujiamini huvuta kuaminiwa siku zote. Watu wanaanza kukuaamini na ulichonacho au usemacho kwa kuona kujiamini kwako. Na hili pia ni tatizo kubwa sana lkatika jamii yetu ya kitanzania. na hili linaanzia katika ngazi ya kifamilia,shuleni na hata maofisini. Mfumo hauandai mtu kuijiamin,hivyo basi unajikuta umekuwa mtu mzima na huna uwezo wa kujiamini kwa
kujielewa zaidi. Mfano mdogo tu,ukipita barabarani ukakutana na msichana mzuri,ukaamua kumsalimia,muangalie usoni mwake,akiitikia ni bahati sana na kama akiitikia unaona tu ni kama anakwambia sitaki kuendelea kukusikiliza hata kama wewe lengo lilikuwa ni kumsalimia tu. Akili zao zimekuzwa kwenye mtazamo hasi kwamba mwanaume akikusalimia njiani anataka kukutongoza. Ukimwambia msichana leo Nakupenda ni wachache sana labda 10% ambaye atabaki na maana hiyo halisi. Neno hilo limechakachuliwa,ukimwambia nakupenda anatafsiri unamtaka kimapenzi. Lakini hii si sawa,nimatokeo mabaya ya mitazamo ya watanzania.
Badilisha Mtazamo wako Badilisha maisha yako.

#Kayson

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment