Mpya
Loading...

Mwanzilishi wa kampuni ya Apple Steve Jobs afariki dunia

Mwanzilishi wa kampuni ya Apple Steve Jobs afariki dunia

 

Mwanzilishi wa kampuni ya Apple aliyevumbua matumizi ya teknolojia ya kisasa ya simu za mkononi na komputa Steve Jobs alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 56.

 
Kifo chake kilichosababishwa na kuugua saratani  kwa muda mrefu kulipelekea  risala nyingi za rambirambi kutoka kwa viongozi wa mataifa mbali mbali,wapinzani wake wa kibiashara na mashabiki kutoka kote ulimwenguni.
Rais wa Marekani Barrack Obama alisema ulimwengu umempoteza mtu aliye na malengo na kwamba atasifika kutokana na uvumbuzi wake wa simu za ipad ambazo hadi wakati wa kifo chake kifaa hicho kilitumika kukitangaza.
Mashabiki waliomboleza nje ya maduka ya Apple kote ulimwenguni wakiwasha mishumaa na kuweka mashada ya maua na kuonyesha picha zake katika simu zao za ipad.
Mmiliki wa kampuni ya microsoft Bill Gates katika risala zake alisema kwa wale waliokuwa na bahati ya kufanya kazi naye ilikuwa ni mtu wa heshima kubwa.
Mwenyekiti wa Google Eric Shmidt alisema Steve alikuwa kielelezo cha kizazi cha mitindo na teknolojia ambayo hakuna anayeweza kuipiku.
Mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Apple Steve Woziniak alisema kifo chake cha Jobs ni kama kile John Lennon au JFK na amekosa hata maneno ya kujieleza.
Kampuni yake ilitoa taarifa kuwa Jobs alikuwa na mkewe na jamaa zake wa karibu wakati akikata roho huko Palo Alto,California.
Jobs alijiuzulu mwezi Agosti kama mkurugenzi na kumkabidhi madaraka Tim Cook.Wachambuzi na wawekezaji wanasema kutokana na azma aliyokuwa nayo Jobs,aliweka mikakati madhubuti kwa kampuni yake kuendelea kustawi hata baada ya kifo chake.
Lakini Apple inakabiliwa na changagamoto kutokana na kutowepo kwa Jobs ambaye alikuwa msingi na ngome ya Apple.Wakinznai wao Google kupitia teknolojia ya Android ya simu wanajizidishia hisa katika soko la simu za Smartphone na kumekuwa na maswali ya ni kipi kikubwa kitakachozinduliwa na Apple katika soko la simu za kisasa.
Jobs aliubadili ulimwengu wa teknolijia katika miaka ya 70 wakishirikiana na rafiki yake Steve Wozniak  wakati Apple 11 ilipokuwa komputa ya kibinafisi ya  kwanza kupata umaarufu sana.
Mwaka 1984 aliboresha uvumbuzi wake kupitia teknolojia ya Macintosh.
Sifa yake ya uasi ilimfanya aondolewe kutoka kampuni hiyo mwaka 1985 lakini alirejea tena mwaka 1997 na miaka michache baadaye akaanzisha ipod,iphone na ipad bidhaa ambazo zilibadili mkondo wa biashara za teknolojia.
Mwaka 2004 aligunduliwa kuwa na na saratani ya kongosho,lakini hilo halikumvunja moyo na kusema kuwa ugonjwa huo unaweza kutibiwa ila afya yake ilizorota mno na baada ya kuchukua likizo mara mbili ya mapumziko ilimbidi ajiuzulu mwezi Agosti mwaka huu kama mkurugenzi mkuu na kuwa mwenyekiti wa kampuni ya Apple.
Steve Jobs ameupatia ulimwengu Apple 11,Mac,ipod,iphone,ipad na Pixar na kubadili maisha na mitindo ya wengi duniani.
Na Hudson Kamoga
Mwenyekiti wa google Eric Schmidt
 Mwenyekiti wa google Eric Schmidt
Rais Barrack Obama wa Marekani
 Rais Barrack Obama wa Marekani
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment